The House of Favourite Newspapers

Kamanda Sirro: Tumekamata Majambazi na Tunaendelea Kukamata!

0

1.Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon N.Sirro akionesha baadhi ya silaha zilizokamatwa.Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionesha baadhi ya silaha zilizokamatwa.2.Kamanda,Sirro akionesha bastola zilizokamatwa katika oparesheni hiyo inayoendelea.Kamanda Sirro akionesha bastola zilizokamatwa katika oparesheni hiyo inayoendelea.3.Simon N.Sirro (kushoto) akizungumza jmbo mbele ya wanahabari.Simon Sirro (kushoto) akizungumza jambo mbele ya wanahabari.4.askari akiziweka mezani baadhi ya silaha zilizokamatwa.Askari akiziweka mezani baadhi ya silaha zilizokamatwa.5.Wanahabri wakichukua tukio hilo.Wanahabri wakichukua tukio hilo.

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia oparesheni yake iliyoanza mwishoni mwa  Desemba, mwaka jana  imefanikiwa kuwakamata majambazi wa kutumia silaha na wanaopora kwa kutumia  pikipiki na wahalifu wengine.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar, Kamanda Sirro alisema katika oparesheni hiyo, Desemba 22, 2015 alikamatwa mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina la Simba S. Said (44) mganga wa kienyeji na mkazi wa Vingunguti jijini na alipohojiwa alikiri kuwafanyia majambazi dawa kabla ya kwenda kufanya matukio ya ujambazi.

Kamada Sirro alisema katika kipindi hicho cha Desemba,  pia jeshi la polisi lilipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa, kuna majambazi maeneo ya Tabata yamekimbilia huko yakiwa na pikipiki ambapo polisi walifuatilia na kufanikiwa kukamata bunduki mbili aina ya PUMP ACTION ambazo namba zake zilikuta zimefutwa  na zikiwa zimekatwa mtutu.

Aliwataja pia watuhumiwa wanane  waliokamatwa kwa kipindi hicho cha Desemba, kuwa ni pamoja na Ibrahim  Mussa (40), Mohammed Shaibu (20), Khamis Jafari (44), Abdulaziz Kikwanda (44), Juma Bakar Msangika (40), Fitina Ramadhan Chaupele (43), Dunia Rashid (50) na Khamis Omar Bankara (36).

Aidha, afande Sirro alisema kwa kipindi cha Januari 7, mwaka huu maeneo ya Gongo la Mboto, Dar jeshi lake lilimkamata jambazi sugu mmoja ambaye kwa kipindi kirefu alikuwa akitafutwa, jambazi huyo anaitwa Mkama Hassan, mkazi wa Mbagala Maji Matitu, Dar na alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na bastola aina ya CHINESE ikiwa imefutwa namba na magazine yenye risasi 7.

Mahojino na mtuhumiwa huyo bado yanaendelea ili kuweza kuwabaini watuhumiwa wengine.

Akizungumzia upande wa pikipiki zilizokamatwa kwa  tuhuma mbalimbali, Sirro alisema jumla ya pikipiki 600 zilikamatwa katika Mikoa ya Kipolisi ya Kinondoni, Temeke na Ilala huku akisisitiza kuwa,  wote wanaoendesha pikipiki wakati taa za barabarani za kuongoza magari hazijamruhusu kupita lazima watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali hata  sehemu ambazo hawaruhusiwi kufanyia biashara za bodaboda.

 NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply