
Dar es Salaam 25 Machi 2023: Asasi isiyo ya kiserikali ya HUDEFO inayojihusisha na usafi na utunzaji mazingira katika kuazimisha siku ya usafi wa kila Jumamosi ya mwisho ya mwezi imefanya jambo la kipekee kwa kufanya usafi na kupanda miti mitaa ya Makuburi Kibangu, Ubungo, Dar.

Akizungumza na Global Tv, Mwanzilishi ya Asasi hiyo, Sara Pima amesema watu wamekuwa wakiyasahau maeneo ya Makaburi Kibangu ambayo nayo yanahitajika kufanyiwa usafi wa mazingira. Mkurugenzi huyo wa HUDEFO aliendelea kusema;
“Naomba nitumie nafasi hii kuishukuru Manispaa ya Ubungo, Serikali ya Mtaa huu , Kata na Wananchi wote wa maeneo haya kwa ujumla kwa kutupa sapoti kwenye zoezi letu hili la leo maana wamejitokeza kwa wingi watu wa rika na jinsi mbalimbali wakiwemo wanawake, wanaume, wazee na watoto wote katika kuunga mkono zoezi hili.

“Vilevile nazishukuru taasisi zote zilizojitokeza kuungana nasi kwenye kampeni hii kama vile Jielimishe Kwanza, Mazingira Plus na Juzza”. Alisema Sara.

Sara amemalizia kwa kusema zoezi hilo kwao ni endelevu na mwezi unaofuata kama kawaida wataenda sehemu nyingine kufanya kama hivyo na kuwaasa wengine kuiga mfano huo.

Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Makuburi Kibangu, Dar, Naima Mdegela ameipongeza HUDEFO kwa kulichagua eneo lake kufanya zoezi hilo kuwaasa wananchi wengine kulinda mazingira na kuiheshimu siku ya usafi wa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kwa kutoendelea na shughuli yeyote mpaka wafanye usafi wa maeneo yao kwanza.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Jielimishe Kwanza na Mdau wa Mazingira, Henry Kazura ameipongeza Asasi ya HUDEFO kwa kuandaa tukio na kuwaalika kushirikiana nao pamoja na kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi kuhusu usafi na utunzaji wa mazingira kwa faida yetu na vizazi vijavyo. Alimaliza kusema Kazura
Kwa mawasilino zaidi kuhusu Hudefo wasiliana nao kupitia
PHONE NUMBER
+255 786 625 969 +255 759 767 602
LOCATION
Ada estate-Kinondoni District opposite Dar Free Market Mall. P.O.Box 80726 Dar Es salaam, Tanzania.