×

Je, Kuna Marehemu Yeyote Aliyewahi Kutoroka?

Mchungaji Ambakisye aliitisha mkutano na waumini wake wenye lengo la kuchangisha pesa kwa ajili ya kujenga ukuta wa kuzunguka makaburi ya kanisa lao.

Mchungaji akawaambia waumini wake kuhusu nia hiyo, nao wakakubaliana kwa pamoja, mchungaji akataka kujua kama kuna muumini mwenye swali.

Muumini mmoja ambaye anajulikana kwa ulevi, akasema: “Mimi nina swali baba mchungaji.”

Mchungaji: “Uliza muumini wangu.”

Muumini mlevi: “Je, kuna marehemu yeyote aliyewahi kutoroka kwa sababu makaburi hayana ukuta?”

Mchungaji: Kimyaaa!

Leave a Comment