
Timu ya Wasichana ya Shule ya Sekondari ya Fountain Gate ya Dodoma, imeibuka mabingwa wa mashindano ya soka ya shule za Afrika ya CAF.
Fountain Gates imetangazwa kuwa bingwa baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa fainali dhidi ya Ecole Omar Ibn Khatab ya Morocco katika mchezo uliochezwa mchana wa leo, April 8, 2023.
Mashindano hayo yaliyowakutanisha mabingwa wa Kanda za Afrika kwa Wavulana na Wasichana, yamefanyika Durban nchini Afrika Kusini.
Haya ni mafanikio makubwa zaidi kwa timu hiyo, ambayo ilipata nafasi hiyo baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano hayo katika Kanda ya Afrika Mashariki na kati (Cecafa).