×

Toto Afrika yapata viongozi wapya

Klabu ya soka ya Toto African ya jijini Mwanza leo imefanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wake wapaya  katika uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya jiji la Mwanza na kufanikiwa kuwapata viongozi ambapo Gasper MwanaLyela ndiye amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa timu hiyo akimshinda Ahmed Waziri Gao katika uchaguzi huo.

Akitangaza uchaguzi huo mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya chama cha soka mkoa wa Mwanza MZFA Alhaji Majogoro amemtangaza Gasper Mwanalyela kuwa mwenyekiti akipata kura 24 huku Juma Mrisho akichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti baada ya kupata kura 40, wajumbe wa kamati waliochaguliwa ni pamoja na Saleh Akida, Hussein Tade,Yusuph Budodi pamoja na Kenneth Shuma.

Akizungumza na Mtandao huu mwenyekiti mpya aliyechaguliwa katika uchaguzi huo Gasper Mwanalyela amesema  anawapongeza wanachama wa Toto African kwa kumchagua “Ninawapongeza wanachama wa Toto kwa kuniachangua niwaahidi kwamba nitahakikisha natengeneza mifumo imara ili klabu yetu iweze kujiendesha kisasa pamoja na kwamba hivi sasa iko katika madaraja ya chini”

“Mpango wa kwanza tunapoingia madarajani ni kutengeneza mfumo imara wa kuiendesha timu hii tunataka timu ikipanda daraja kucheza ligi kuu isiteremke daraja kila wakati kwani hilo jambo linachosha, pia tutafanya marekebisho ya katiba ili wapa majukumu wale wanachama wetu wanaolipia ada ya kila mwezi maana tunahitaji kuiendesha klabu hii kwa umoja na mshikamano”

Toto African ilishuka mpaka ligi daraja la nne ngazi ya wilaya ambapo Uongozi ulioingia madarakani unalo jukumu la kuhakikisha klabu hiyo inarejea katika soka la Ushindani hapa nchini.

Leave a Comment