×

Litombo Aaga FAR Rabbat

IMEFAHAMIKA kuwa Simba imekamilisha usajili wa beki wa beki wa FAR Rabbat ya nchini Morocco, Bangala Litombo atakayekuja kuchukua nafasi ya beki mmoja wa kati wa Simba.

 

Simba imepanga kuiboresha safu yao ya ulinzi ambayo tayari imekamilisha usajili wa beki wa kulia Israel Mwenda kutoka KMC. Litombo tayari ameiaga klabu yake hiyo ambayo kwa sasa inafundishwa na kocha wa zamani wa Simba, Sven Vandebroeck kwa ajili ya kuja nchini kumalizana na Simba inayohitaji saini ya nyota huyo.

 

Mmoja wa mabosi wa timu hiyo, ameliambia Championi Jumatatu, Simba imefi kia muafaka mzuri na Litombo ambaye muda wowote atatua nchini kwa ajili ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

 

Bosi huyo alisema kuwa kutua kwa Litombo kutamuondoa beki mmoja wa kati ambaye ataagwa siku ya Simba Day. Aliongeza kuwa Litombo atasaini mkataba baada ya yeye mwenyewe kuonekana kuhitaji kujiunga na Simba.

 

“Usajili wa Litombo ukikamilika, basi beki mmoja wa kati aidha Wawa Pascal au Joash Onyango safari itamkuta ili ampishe beki huyo Mkongomani.

 

“Uongozi umepanga kumuandalia utaratibu mzuri wa kumuaga Wawa ambaye mkataba wake umemalizika wa kuendelea kuichezea Simba mwishoni mwa msimu huu.

 

“Litombo wamefi kia muafaka mzuri na Simba, hivyo ndani ya wiki hii huenda akatua nchini tayari kwa safari ya kambi ya nje ya nchi kwa ‘pre seasson’,”alisema bosi huyo.

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ hivi karibuni alisema kuwa “Simba imepanga kukifanyia maboresho kikosi katika kuelekea msimu ujao kwa kufanya usajili wa kimyakimya kwa hofu ya kuzidiwa ujanja na klabu nyingine”.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave a Comment