
Dar es Salaam 17 Machi 2022: Wizara ya Afya na Vodacom Tanzania wamekabidhi vyumba vipya 6 baridi ambavyo vitatumika kuhifadhia chanjo.
Vifaa hivyo ambavyo vina thamani ya zaidi ya TZS 600 Milioni vilivyotolewa na Vodacom Tanzania Foundation na Vodacom Group, vitahakikisha chanjo zinahifadhiwa kwa usalama hivyo kuimarisha mpango wa Taifa wa chanjo nchini.
Msaada huo uliotolewa na Vodacom Foundation na Vodacom Group umekuja katika wakati ambao bara la Afrika linapitia changamoto za uhifadhi wa chanjo kwenye nchi mbalimbali. Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya duniani (WHO), Kanda ya Afrika kwenye nchi 34 za Afrika umebaini kuwa, katika asilimia 31 ya nchi hizo, zaidi ya asilimia 50 ya wilaya zake zina changamoto za usambazaji wa chanjo kutokana na ukosefu wa vifaa vya kuhifadhia madawa hayo.

Usimamizi wa mnyororo mzima wa vifaa baridi ni sehemu muhimu ya kuhakikisha usambazaji salama na mzuri wa chanjo. Chanjo zinahitaji majokofu imara ambayo yanakidhi mahitaji fulani ya joto, kutoka mahali pautengenezaji hadi hatua ya mwisho ya usambazaji. Ikiwa mnyororo huu utavunjika wakati wowote inaweza kuathiri ufanisi mzima wa chanjo na kuzifanya zisiwe na uwezo wa kuzuia maradhi.

“Kama serikali, tunashukuru kuendelea kuungwa mkono na sekta binafsi katika kufikia malengo ya sekta ya afya Tanzania na Vodacom wamekuwa wadau wakubwa wa maendeleo ya jamii. Ninaamini mchango huu kutoka Vodacom Tanzania Foundation utasaidia sana katika kulinda chanjo dhidi ya athari zinazoweza kuepukika.
“Nawasihi watumishi wa sekta ya afya tu kuvilinda vifaa hivyo lakini pia kutumia nafasi na ushawishi wetu kuhamasisha jamii kujitokeza kupata chanjo,” alisema Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Vodacom Tanzania Foundation, Harriett Lwakatare, alisisitiza dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono juhudi za serikali kufikia malengo endelevu ya SDG kwa kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia sekta ya afya.
Juhudi hizi zinatekelezwa kwa ushirikiano na serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na washirika wengine wa maendeleo. Juhudi hizi ni pamoja na kuanzishwa kitaifa kwa mfumo wa usafiri wa dharura ya ‘m-mama’ –program ya kiafya ya Vodacom kuhamasisha afya ya uzazi salama kupitia mradi wa ‘Fistula Inatibika’ na msaada wa kujifungua kabla ya muda na kadhalika.
“Tunafuraha kwa mara nyingine tena kufanyakazi kwa ukaribu na Wizaraya Afya katika kuunga mkono mpango wa Taifa wa chanjo.

Mitambo hii ya baridi kali iliyofungwa hapa Dar es Salaam na Zanzibar itaisaidia serikali katika uhifadhi na usambazaji wa chanjo za kuokoa maisha, zikiwemo zile zinazotumika kama chanjo kwa watoto,” alisema Lwakatare.
Hilda Bujiku, Mkurugenzi wa Fedha kutoka Vodacom kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Philip Besiimire alieleza dhamira ya kampuni hiyo katika kuharakisha mafanikio ya SDGs kwa kuimarisha ushirikiano katika nyanja za afya, elimu, kilimo na ushirikishwaji wa kifedha.
Aidha alihimiza mashirika mengine kuongeza kasi ya ushirikiano baina ya sekta za umma na binafsi kwa manufaa ya nchi nzima.
About Vodacom Tanzania Foundation
The Vodacom Tanzania Foundation is the CSR arm of Vodacom Tanzania PLC with the mandate to provide public benefit to vulnerable groups with a focus on women & youth. The Foundation combines charitable giving and leverages on mobile technology to provide solutions to social challenges. Working with local non-governmental organizations and the government, Vodacom Tanzania Foundation has supported over 2 million beneficiaries to date and hasinvested over Tsh 11 Billionin improving the lives of Tanzanians.
For further information, please visit: https://vodacom.co.tz/foundation