
Mtangazaji na Mwanahabari maarufu wa Mkoa wa Morogoro, Emmanuel Victor maarufu kwa jina la Imma One amefariki dunia kwa ajali mbaya mkoani humo.
Emmanuel aliyekuwa akiripoti Kituo Abood Media mjini Morogoro amefariki usiku wa kuamkia leo Alhamisi Aprili 20, 2023 maeneo ya Simon katika Barabara Kuu ya Morogoro na Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mashuhuda na video za eneo la tukio, mwanahabari huyo alikuwa akiendesha gari ndogo aina ya Toyota IST na alikuwa akielekea nyumbani kwake maeneo ya Mkambalani mjini Morogoro.