×

Kuzimu Na Duniani-15

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Utakuta baa nzuri sana, lakini viti vitupu muda mwingi. Ukweli wa hapo ni kwamba, eneo hilo si kwamba wateja hawataki kuingia bali kuna majini nayo yanapenda kukaa kwenye baa hiyo wakifanya mambo yao ya kila siku.
SASA ENDELEA…

Sasa hapo, wewe binadamu wa kawaida, utasema viti vitupu kwenye baa lakini kumbe vina watu wamekaa na wanaendelea na mambo yao huku wakikuangalia. Ukisema uende roho inasita au unajikuta miguu inakata kona na kwenda kukaa sehemu nyingine kabisa. Hapo ujue miongoni mwa hao majini kuna mmoja ambaye amekuelekeza kukaa huko.

Na dalili kubwa kwamba baa unayoingia siku hiyo wamekaa majini, hasa kama baa hiyo itakuwa ni ile uliyoizoea siku zote ni kwamba, utajikuta umekaa sehemu ambayo hujaizoea. Na hili utagutuka baadaye sana ukiwa umeshakaa na kuendelea na vinywaji.
Kitakachokutokea, utajiuliza ghafla kwa nini mimi leo nimekaa eneo hili ambalo huwa silipendi kabisa.

Kuna mambo mengi sana katika yasiyoonekana. Wengi wamekuwa wakilalamika biashara fulani haiendi vizuri bila kujua kwamba, majini yameingilia kati.

Mfano, mtu anafungua gesti nzuri sana, ipo mahali pazuri sana, tena si ajabu ni jirani kabisa na kituo kikuu cha mabasi yanayokwenda mkoa, lakini gesti hiyo haiwagi na wateja hata siku moja. Kama kuna vyumba ishirini, vinne vitapata watu, vinavyobaki vinalala vyenyewe.

Ujue hapo kuna majini ambao wameamua kupiga kambi kwenye gesti hiyo. Kinachotokea ni kwamba, majini yamekuja duniani na yanataka kufanya kazi fulani, sasa wakakae wapi, wanapata mwafaka wa kukaa kwenye gesti hiyo. Wanagawana vyumba mpaka vinabaki hivyo vinne tu.

Sasa kazi yao kubwa hao majini ni kuhakikisha mmoja wao, anasimama nje kuhakikisha wateja hawaji baada ya nyumba vinne kujaa.

Wengi utawasikia wakisema labda gesti hiyo, huenda nyumba iliyotumika iliwekewa madudu. Kwa hiyo tajiri wa gesti anatafuta mganga wa kienyeji eti kwenda kuagua wakati uganga wenyewe unaongozwa na majini.
Katika hali kama hii, mwaguzi mkubwa si mganga wa kienyeji bali viongozi wa dini mbalimbali.

Basi, bethidei ilifanyika, lakini kwa utaalam wa kimajini muziki wa baa ukawa unaleta matatizo ya kukatikakatika mara kwa mara hivyo sisi muziki wetu ukawa unasikika sawasawa lakini bila wateja kujua hilo kwani na wao walionekana kuendelea na shughuli zao.

Halafu hapa pia nataka kusema kwamba, huwa inatokea, unakuta baa imepoa sana! yaani unakwenda baa, hakuna muziki wa redio wala wa tivii lakini vitu vyote vipo, yaani redio ipo na tivii ipo.

Mara nyingi katika mazingira kama haya ujue kuwa, kuna majina wapo hapo wanaendelea na shughuli zao. Pengine wamefika kula na wanaongea mambo yao au wameamua tu kutumia baa hiyo kuongea mambo yao hata kama hawali chochote.

Zipo kumbi za harusi nazo zinadoda. Ukumbi upo pazuri, maegesho ya magari yapo, tena upo karibu na barabara lakini haupati wateja. Ukiona hivyo ujue kuna majini nao hufanya sherehe zao siku za mwishoni mwa juma au wikiendi.
Kawaida ya majini ni hiyo, wakiweka kambi mahali kwa hapa duniani huwa hawana tabia ya kuhamahama, mara huku, mara kule.

Tabia hii imekuwa ikiwaumiza binadamu wengi kwa maana ya kuingiliwa katika maeneo yao ya biashara. Wako watu wanapanga baa ili kufanya biashara, baada ya mwaka mmoja wanahama, anakuja mwingine, baada ya mwaka mmoja anahama. Basi inakuwa hivyohivyo.

Hali hii pia hutokea kwenye nyumba za kupanga. Kuna nyumba wapangaji wanahama kila mwaka. Ukiwauliza wanaohama wanaweza kukupa sababu nyingine kabisa. Lakini ukweli ni huohuo.

Ila sasa, kwenye nyumba mara nyingi majini hutumia vyumba vilevile ambavyo binadamu wengine wa kawaida hutumia. Ndiyo maana kuna watu hulalamika kwamba, wanaamka wakiwa wamechoka sana. Mwili mzito sana, usingizi haujaishi sawasawa au mpaka wengine wanasema hawapati usingizi wa kutosha.

Mara nyingi, ukiwa unaishi na majini kwenye nyumba moja wao wana tabia ya kumkandamiza binadamu. Mfano, ukilala kitandani kama na yeye jini chumba chake ni hichohicho, basi ukishalala anakubeba na kukulaza sakafuni.

Kama wakirudi na kukukuta sebuleni, pia wana tabia ya kulalia au kumkalia mtu kwenye mapaja. Sasa kama unaangalia tivii ukitaka kujua umekaliwa na majini, utajikuta unapenda kuzima tivii ili ukae kimya au mara nyingine utapenda kubadilibadili vituo vya tivii bila kujua ni kituo gani hasa unataka kuangalia.

Unapokwenda kuoga, unaweza kukuta maji ndoo nzima lakini umemaliza yote na bado sehemu fulani za mwili zina povu la sabuni. Hapo ujue umeoga na mmoja wa majini.
Kwa majini haya yanayopenda kukaa na binadamu kwenye makazi mamoja ni mara chache sana kukufanyia vituko au visa ambavyo mtu utajua. Ila ni kwa kutumia vigezo hivyo vidogovidogo.

Fuatilia sana tabia za kupoteza vitana nyumbani. Si vitana tu, vitu vyovyote vidogovidogo.
Usikose kusoma mwendelezo wiki ijayo katika gazeti hilihili.

Mara kalamu haipo, mara kuna CD ya muziki ilipotea, mara kuna glasi au kijiko hakionekani! Ujue unaishi nyumba moja na majini.

Kupotea kwa vitu hivyo marra nyingi kuna sababishwa na wao kutovipenda vitu hivyo. Unaweza kununua kitana, wao, hasa yule unayeishi naye kwenye chumba kimoja hakipendi kitana hicho. Kwa hiyo anakichukua na kukitupilia mbali. Kwa upande wa wanawake, wengi hujikuta wakipotelewa na…

Je, wewe msomaji unajua kilichotokea? Usikose kusoma wiki ijayo kwenye gazeti hili.

Leave a Comment