×

Baba P… Baba Pili… Baba Pilima!-12

ILIPOISHIA IJUMAA WIKIENDA:
“Haitatokea baby. Unajua baby mtu ukitoka kufanya mambo kama haya halafu ukaongea kwa simu mtu anaweza kujua, maana kuhema kunakuwa kwingi ndiyo maana sitaki kupokea,” alisema mama Pilima, baba Pili akawa amemuelewa.

“Oke, nimekuelewa mama Pilima, lakini kuna jambo ambalo nataka kuzungumza na wewe kidogo,” alisema baba Pili…
SHUKA NAYO MWENYEWE SASA…

“Liseme tu baba Pili mimi niko tayari kukusikiliza…”
“Unajua mimi nafahamu ni kwa nini wewe ulikuwa hupokei simu wala hutaki mawasiliano na mimi…”

“Kama kweli ulikuwa unafahamu niambie ni kwa nini?”
“Ulibanwa mama Pilima…”
“Ndiyo nilibanwa, si nilikwambia lakini…hilo ndilo unalolifahamu?”
“Liko zaidi mama Pilima, ila oke…sasa siku nyingine uwe makini sana…”
“Na nini baba Pili..?”
“Unajua mimi ni baba Pili…”

“Najua baba Pili kuwa wewe ni baba Pili…enhee..?”
“Oke, lakini kuna pacha wangu anaitwa baba Pilima.”
Mama Pilima alitumbua macho, akavuta pumzi kwa ndani kisha akajiinamia huku uso wake akiuweka kwenye kiganja cha mkono…

“Baba Pili,” aliita mama Pilima…
“Niambie nakusikiliza…”
“Nisamehe sana! kama ni kweli, ina maana unajua kila kitu…lakini si kosa langu ndiyo maana hata wewe mwenyewe umesema ni pacha wako…
“Lakini naumia sana baba Pili na kitu kimoja…”
“Kitu gani hicho?”

“Nakulaumu…ina maana umekuwa tayari kabisa wewe na ndugu yako kutembea na mwanamke mmoja?”

“Hilo lisingeweza kuzuilika kwani ulitaka mwenyewe…”
Mama Pilima alishtuka kuambiwa alitaka mwenyewe…
“Nilitaka mwenyewe kwa njia gani?”
“Kwani mazingira yenyewe hayakukuonesha kuwa, yule mwanaume si mimi? Unajua ikitokea mimi nakutana na mwanamke aliyefanana na wewe, au ni pacha wako, nitajua tu. Kuna mazungumzo yatakuwa yanaachana.”

Mama Pilima alijikuta katika aibu kubwa baada ya kujua kuwa, mambo yake ya siri yamejulikana…
“Daa! Nimeumbuka mwanamke! Hivi kumbe siku zote hizi ananitafuta lakini anajua kila kitu! Anajua kwamba natembea na pacha wake! Da! Nimevuruga maisha na nimejivunjia rekodi…

“Sikuwa tayari kuwa na uhusiano wa kimapenzi zaidi ya mwanaume mmoja lakini ghafla tu imetokea nimekuwa na mapenzi na wanaume watatu. Baba Pili, baba Pilima yule na baba Pilima mume wangu… Da!” aliwaza sana moyoni mama Pilima.
Lakini moyoni mwanamke huyo alikiri kwamba, wanaume hao wawili ni kiboko kwenye kitanda. Alitamani hata mume wake angekuwa hivyo…

“Kweli ni mapacha, hata mapigo yao ni ya kipachapacha tu,” alisema moyoni mama Pilima.

“Sasa itakuaje baba Pili?” aliuliza mama Pilima…
“Kuhusu nini mama Pili..?”
“Mimi nimekubali kosa, ina maana ndiyo basi tena mimi na wewe au?”
“Nitakujibu,” alisema baba Pili akitoka kitandani na kuanza maandalizi ya kuondoka ndani ya chumba hicho. Mama Pilima naye alijiandaa kwa kuondoka.
***
Alipoachana na baba Pili, mama Pilima hakutaka kukutana na baba Pilima feki, alirudi nyumbani huku uso wake ukijaa aibu kwa kila aliyekutanisha naye uso njiani.
Alifikia kwenye kochi kubwa, akajilaza amechoka ile mbaya. Lakini zaidi sana ni kwamba, atawezaje kuwa mbali na wanaume hao wawili mapacha?

“Nikisema nibaki na baba Pili, baba Pilima naye yuko vizuri sana. nikisema nibaki na baba Pilima, hivyohivyo kwa mwenzake. Hili limeshatokea, kama watakubali nitabaki na wote tu,” aliwaza moyoni mwanamke huyo mwenye umbo nambari nane.

Aliishika simu yake na kubadili muundo wa majina. Baba Pilima feki akamsevu kwa jina la baba P, baba Pili akaendelea kuwa hivyohivyo. Kwa hiyo kwenye simu yake kuwa na baba P, baba Pili na baba Pilima ambaye ni mume wake.

Kwa upande wake, baba Pilima alipokuwa nyumbani kwake alimfikiria mama Pilima kwa maana kwamba, kwa vile si mkewe, aliamua kuendelea naye kimapenzi hata kama pacha wake naye ataendelea naye…

“Kwani mi ni mke wangu yule? Dawa yake ni kupita tu kila nitakapojisikia,” alisema moyoni.
***
Kwa upande wake, baba Pilima hali ilikuwa tofauti kidogo. Yeye alijua penzi lake na mama Pilima limekwisha ndiyo maana mwanamke huyo hakumpokelea simu.
Lakini kwa maneno aliyoambiwa na pacha wake, baba Pili alijua hana chake kwa mama Pilima. Akajuta kwa nini alimsimulia kisa chote pacha wake, angemficha maana wakati anakutana na mama Pilima alijua amemchanganya na baba Pili…

“Da! Ama kweli hakuna siri ya watu wawili. Siri inayodumu ni ile ya wewe peke yako. Sasa kumshirikisha pacha imekuwa nongwa. Je, tungezaliwa kwa kupishana miaka miwili?” alisema moyoni baba Pilima.
***
Usiku, baba Pilima aliwasili nyumbani kwake na kufikia sebuleni. Baada ya kuvua viatu na soksi, alizungumza na mkewe, mama Pilima…

“Anko wako kanipigia simu, anasema nimpigie, ana shida na mimi…sasa simu yangu haina pesa, niazime ya kwako,” alisema baba Pilima huku akiwa tayari ameshanyoosha mkono kuipokea.
Je, nini kilitokea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda, siku ya Jumatatu.

Leave a Comment