×

Waziri Mkuu Akutana na Wafanyabiashara Kariakoo, Atoa Maagizo – Video

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam Leo Mei 15, 2023

 

Kufuatia mgomo wa wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Mei 15, 2023 amesafiri kwa dharura kutoka Dodoma hadi Kariakoo kwa lengo la kuwasikiliza wafanyabiashara hao.

Awali, taarifa zilieleza kuwa Waziri Majaliwa atakutana na wafanyabiashara hao Jumatano ya Mei 17, 2023 lakini kufuatia wafanyabiashara hao kuendelea kushikilia msimamo wao, amekutana nao leo huku akieleza kwamba watakutana tena na kujadiliana kwa kina Jumatano.

Majaliwa baada ya kusikiliza kero za Wafanyabiashara wa Kariakoo ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kusitisha shughuli za Kikosi Kazi cha Kukusanya Kodi (Task Force) ambacho amesema kinatumika kufanya kamatakamata na wakati mwingine kuchukua rushwa.

 

Waziri Mkuu Majaliwa akiwa Kariakoo, amesema:

“Tuna taarifa kuwa kuna kikosi kazi kimeundwa kinazunguka huko, Rais alikemea Vikosi Kazi (Task Forces) kwasababu vinatumika kuwasumbua wafanyabishara na kuomba pia rushwa, naagiza hiyo task force isitishwe mara moja.

“Task force hii ndiyo inaendesha kamatakamata kila siku, Kamishna wa Mapato ya Ndani TRA naagiza isitishwe, kanuni zipo sheria zipo zinatuelekeza namna ya kulipa kodi, kamatakamata hii inafukuza Wafanyabiashara Kariakoo na mbaya zaidi mnawakamata hadi Wageni kutoka nje.”

Leave a Comment