×

Kocha USM Alger Alia Na Refa Fainali ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika

KOCHA wa USM Alger, Abdul Benchikha, alisema wazi kuwa licha ya timu yake kupata ushindi wa mabao 1-2 ugenini mbele ya Yanga, ila kuna vitu hakuridhishwa navyo.

Benchikha alisema mwamuzi alikuwa bora mwanzoni mwa mchezo huo, lakini kipindi cha pili akabadilika na kuamua kuwa upande wa Yanga kwenye baadhi ya matukio.

Kauli ya kocha huyo inakuja baada ya kukiongoza kikosi chake kupata ushindi huo katika fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa juzi Jumapili Uwanja wa Mkapa, Dar.

“Kipindi cha pili mechi haikuwa nzuri upande wetu kwa sababu hata refa naye alianza kuonekana kupendelea timu ya nyumbani (Yanga), hii ni kawaida ukicheza ugenini.

“Lakini nimecheza dhidi ya timu nzuri yenye wachezaji wenye vipaji kuanzia nafasi ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji.

“Tunarudi Algeria lakini bado mechi haijaisha, ni asilimia 50 kwa 50. Bado tuna kazi ya kufanya Algeria kwa sababu katika mechi ya marudiano Yanga hawana cha kupoteza, watacheza wanavyojua ili wapate matokeo mazuri,” alisema kocha huyo.

STORI: ISSA LIPONDA

Leave a Comment