×

Ripoti Mpya Ya Kifo Cha Nusura Mambo 13 Mazito, Haki Za Binadamu Wamaliza Utata – Video

Aliyekuwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Nusura Hassan Abdallah.

Ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala (THBUB) imetoa ripoti baada ya uchunguzi wa kifo cha aliyekuwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Nusura Hassan Abdallah kilitokana na shambulio kali la kupanda kwa Sukari na upungufu wa Damu mwilini na siyo ajali kama ilivyoripotiwa hapo awali na baadhi ya watu.

Ripoti inasema kuwa kifo cha Nusura hakiusiani na Ajali ya gari ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – OR, TAMISEMI (Afya) Dkt. Festo John Dugange.

Tume imeeleza ajali ya Dkt. Dugange ilitokea usiku wa kuamkia Aprili 26, 2023 wakati Aprili 27, 2023 Nusura alisafiri kuelekea Moshi akiwa mzima wa Afya kabla ya kukutwa na mauti Mei 1, 2023 akiwa Hospitali alipokuwa akitibiwa baada ya kumaliza kula na kuanza kuumwa

Ripoti imeeleza mabaki ya chakula walichokula Marehemu Nusura, mchumba wake na mpwa wa mchumba wake; na matapishi yaliwasilishwa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi ulionesha kutoonekana kwa dalili yoyote ya kuwemo kwa sumu.

Tume haikuweza kuthibitisha mtu yeyote kuhusika na kifo cha Marehemu Nusura Hassan Abdallah kutokana na vielelezo vya Hospitali ya Faraja, Mkemia Mkuu wa Serikali, na maelezo ya mengine ya mashahidi.

Leave a Comment