×

Video: Mama Amwaga Machozi Akimlilia Rais Samia, Atimuliwa Kwake Kinyama – ”Mpinzani Wangu Ana Pesa”…


Mwanamke mmoja mjane, mkazi wa Gongo la Mboto, Majohe jijini Dar es Salaam amemlilia Rais Samia Suluhu Hassan akitaka amsaidie kutokana na kufanyiwa ‘umafia’ na benki moja nchini.

Amesema alienda kukopa kwenye benki hiyo na kuandikisha nyumba yake iliyopo Buguruni kama dhamana endapo atashindwa kulipa mkopo lakini cha ajabu, aliposhindwa kulipa, benki hiyo ilienda kupiga mnada nyumba yake nyingine aliyokuwa akiishi ambayo haikuwa kwenye makubaliano.

Amesema, benki hiyo ilituma watu wapatao 30 kwenda kutoa vyombo vyake kwa nguvu na kusababisha aibiwe vitu vingi, kibaya ni kwamba alihamishwa kwa nguvu bila hata kupewa notisi.

Leave a Comment