
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchema amesema Serikali itaendelea kununua na Kusambaza Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi kwa vituo vyote vya Umma vya Huduma za Afya, ambapo jumla ya Tsh. Bilioni 544.2 pamoja na Tsh. Bilioni 487.5 zimetolewa kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ambapo nia ya Serikali ni kuona huduma za Afya zinaimarika
Hivyo katika Mwaka wa fedha 2023/24 Serikali itaendelea kutenga Fedha kwa ajili ya kuboresha Huduma za Afya ikiwemo kuipatia mtaji MSD ili ifanye kazi kama Bohari ya Dawa na sio kitengo cha ununuzi wa Dawa Serikalini.