×

Panga Zito Lapita Simba Waachana na Makocha wao Watatu

KAZI imeanza ndivyo unavyoweza kusema kuelezea kile ambacho kinaendelea ndani ya kikosi cha Simba hii ni baada ya jana Alhamisi kutangaza rasmi kuachana na makocha wao watatu kama sehemu ya maboresho ya benchi lao la ufundi kuelekea msimu ujao wa 2023/24.

Simba imeachana na kocha wa makipa, Chlouha Zakaria kocha wa viungo na utimamu wa mwili, Kelvin Mandla na Daktari na Mtaalamu wa Viungo, Fareed Cassiem.

Simba kupitia akaunti zao rasmi za mitandao ya kijamii walitoa taarifa iliyoeleza: “Asante kocha wetu wa magolikipa, Chlouha Zakaria kwa muda wote uliokuwa sehemu ya benchi letu la ufundi. Tunakutakia kila la kheri katika maisha yako mapya nje ya Simba, pia tunawashukuru kocha wa viungo Kelvin Mandla na kwa mtaalamu wa viungo Fareed Cassim kwa muda wote waliokuwa nasi kuhakikisha wanawatibu wachezaji wetu. Tunasema asante.”

Akizungumzia fagio hilo Meneja wa habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema: “Tuliweka wazi kuwa tunatarajia kufanya maboresho makubwa ya benchi letu la ufundi na kikosi chetu kwa ajili ya kurudisha nguvu yetu na ushindani wa kutwaa mataji, tunawashukuru wale wote waliokuwa safarini pamoja nasi na kuwatakia kila la kheri katika maisha yao mapya na nguvu kubwa tunaielekeza kujenga timu ya mataji.”

Stori: Joel Thomas

TAMU, CHUNGU BAJETI ya SERIKALI/ VITANZI VINNE kwa BALOZI CCM/MBOWE ATOA OMBI kwa SERIKALI..

 

Leave a Comment