×

Rostam, Kitila Wamvaa Mbowe kwa Kauli za Ubaguzi – Video

MFANYABIASHARA maarufu nchini Tanzania, Rostam Azizi, na mbunge wa Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo, wamemshukia vikali Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kwa kutoa kauli za ubaguzi dhidi ya Wazanzibari kwenye mjadala unaoendelea wa uwekezaji binafsi katika bandari ya Dar es Salaam na kumshangaa mwanasiasa huyo kwa kuleta siasa za ukaburu kwenye jambo la kiuchumi na kibiashara.

Bila kumtaja Mbowe kwa jina, Rostam na Kitila wameonesha kukerwa na kushtushwa na kauli za kibaguzi ambazo Mbowe amezitoa dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa, kwa kuhusisha asili yao ya Zanzibar na maamuzi ya uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam.

Kauli hizo za kibaguzi za Mbowe, ambazo zimerudiwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Wilibrod Slaa, zimechochea mjadala wa kibaguzi wa wanaojiita Watanganyika dhidi ya Wazanzibari kwenye suala la bandari ya Dar es Salaam.

“Hizi siku za karibuni nimekuwa nasikiliza huu mjadala kuhusu uendeshaji wa bandari (ya Dar es Salaam). Sina tatizo na watu kukosoa vitu. Lakini kilichonitatanisha, kunisikitisha na kunisononesha na kunitisha ni sura ya mjadala wenyewe. Ukachukua sura ya kisiasa ya ushabiki na hata hao viongozi walioamua kutumia siasa katika hili jambo wakahusisha na dini,” Rostam alisema kwenye mdahalo wa kitaifa uliofanyika Dar es Salaam.

ROSTAM AZIZ ATEMA CHECHE SAKATA la BANDARI, AFICHUA MAZITO kwa UCHUNGU AKILAUMU SIASA na UKABILA…

Leave a Comment