
Mbunge wa Geita vijijini Joseph Kasheku ‘Musukuma’ amesimama na kutoa ya moyoni kuhusu afisa mmoja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) aliyemtaja kwa jina la Bw. Njau kutokana na tabia yake ya kuwaonea wafanyabiashara wa mkoa wa Geita kwa kuwafanyia vitendo ambavyo ni kinyume na sheria na hivyo wafanyabiashara hao kulazimika kufunga biashara zao na baadaye afisa huyo hufungua biashara yake binafsi.
Musukuma ameitaka serikali kuchukua hatua za haraka kukabiliana na afisa huyo kabla wananchi hawajaamua kuchukua hatua, pia amependekeza kwamba kama afisa huyo bado ni mzuri basi ni bora wamchukue na kumhamishia sehemu nyingine.