×

Kipa Simba Azipambanisha Azam, Singida Azungumza na Spoti Xtra

Beno Kakolanya.

BAADA ya mkataba wake kugota mwisho ndani ya kikosi cha Simba, kipa Beno Kakolanya ameziingiza vitani Azam FC na Singida Fountain Gate zinazotajwa kuwania saini yake.

Kipa huyo alikuwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kilichopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger wa kufuzu AFCON 2023, ilikuwa Juni 18.

Mtu wa karibu wa Kakolanya, aliliambia Spoti Xtra kuwa, kipa huyo ana ofa kutoka timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara zilizo ndani ya tano bora.

“Kakolanya kuna timu ambazo zipo kwenye mazungumzo naye hapa Bongo na muda wowote anaweza kutambulishwa ikiwa watafikia makubaliano mazuri.

“Miongoni mwa hizo timu zilizo ndani ya tano bora ni Azam FC, Singida pamoja na Namungo, hivyo ni suala la muda tu,” alisema mtu huyo.

Nyota huyo ndani ya kikosi cha Simba alipata nafasi kucheza kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara 2022/23 aliposepa na dakika 135.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA | SPOTI XTRA

SIKIA REKODI za KOCHA MPYA wa YANGA, TIMU KUBWA ALIZOFUNDISHA, MAFANIKIO ALIYOYAPATA…

Leave a Comment