
Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamisi Athumani Munkunda na kumteua Mobhare Holmes Matinyi kuchukua nafasi hiyo
Pia uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Abel Yeji Busalama umetenguliwa, na nafasi hiyo itachukuliwa na Hashim Shaibu Mgandilwa, ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini
Aidha, James Wilbert Kaji ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini
