



Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ametembelea kliniki ya Biashara na kupata nafasi ya kusalimiana na Maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanaoshiriki katika Kliniki hiyo iliyomo ndani ya Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam leo tarehe 06. 07. 2023.
Sambamba na Mstaafu Kikwete pia Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Kariakoo Bw. Martine Mbwana aliweza kutembelea Kliniki hiyo na kupatiwa Maelezo kutoka kwa Maofisa wa TRA juuu ya masuala mbali mbali ya kodi katika Banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)