×

Gamondi Aifumua Yanga Nje Ndani Azungumza Kuelekea Msimu Mpya

Miguel Gamondi

KOCHA mpya wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa malengo yake ni kuhakikisha kuwa anawatengeneza wachezaji wake kuweza kucheza zaidi ya nafasi moja, lakini wote wawe wanauwezo wa kuleta ushindani utakaokuwa na msaada ndani ya timu.

Gamondi ambaye ni raia wa Argentina tayari ametua nchini tangu Ijumaa iliyopita kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya akiwa na Yanga mara baada ya Nasreddine Nabi kuondoka.

Akizungumza kuelekea msimu mpya ndani ya Yanga, Kocha Gamondi alisema kuwa moja kati ya mambo ambayo anayatamani ni kuona wachezaji wake wakiwa wanauwezo wa kucheza zaidi ya nafasi moja huku pia akiwekea mkazo wa kuwa na wachezaji ambao wanaweza kutoa changamoto kwa wengine ili ushindani uwe mkubwa.

“Ili kuupata ubora ambao ni mkubwa ndani ya timu lazima tuhakikishe kuwa tunapata wachezaji ambao wataleta ushindani mkubwa kwa wachezaji wenzao na hiyo itakuwa ni chachu kubwa kwa kuleta mafanikio ndani ya timu kwa kuwa tutanufaika na ushindani wao.

“Kwa upande wa nafasi pia tunatakiwa kuwa na wachezaji ambao wanaweza kucheza nafasi zaidi ya moja ili kuwa na matumizi ya ziada pale ambapo kuna shida ama tatizo, kikubwa ni sisi kupata mafanikio na ndio maana mipango lazima iwepo,” alisema kocha huyo.

Yanga imepanga kuanza kambi ya kujiwinda na msimu ujao leo Jumatatu pale Avic Town iliyopo Kigamboni jijini Dar.

Na Marco Mzumbe, Championi

WANNE WAFUNGA USAJILI YANGA/ BAADA ya MALONE, VYUMA 3 VIMEBAKI SIMBA, MIQUISSONE ATAJWA…

Leave a Comment