×

Baada Ya Kusaini.. Kaze Aanza na Carlinhos Yanga

CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga ambaye amepewa dili la miaka miwili, amesema kuwa ni lazima ambadilishie mbinu kiungo wake Carlos Carlinhos za kuwalisha mipira mingi washambuliaji wake.

 

Yanga ikiwa imecheza mechi tano za ligi, imefunga mabao saba na kufungwa bao moja. Kinara wa pasi za mwisho ni Carlinhos akiwa ametoa pasi mbili na kufunga bao moja na pasi zake zote alizotoa alikuwa pembeni ya uwanja kwa kuwa alizitoa kupitia kona.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kaze alisema kuwa washambuliaji wake wanashindwa kufunga mabao mengi kwa kuwa wanapata pasi za aina moja, mbinu ambayo imegundulika na wapinzani wao.

 

“Ujue ili ufunge ni lazima uwe na walishaji wa mipira kutoka sehemu tofauti ikiwa ni pamoja na katikati, kulia na pembeni. Kwa namna ambavyo nimekiona kikosi cha Yanga, wengi wamekuwa wakifunga kwa mabao ya pembeni.

 

“Nitakachokifanya ni kuwabadilishia mbinu hao wanaowalisha washambuliaji wangu ambapo huyo Carlinhos amekuwa akitokea pembeni, sasa atakuwa na kazi nyingine ya kufanya ndani ya uwanja.

LUNYAMADZO MLYUKA NA IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

Leave a Comment