
Rais wa Hungary, Katalin Novák, amewasili nchini Julai 17, 2023 kwa ziara ya kikazi ya siku nne kuanzia tarehe 17 – 20, Julai 2023.
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Novák amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.)

Akiwa nchini, leo tarehe 18 Julai 2023 Novák anatarajia kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na kufanya mazungumzo rasmi na baadae viongozi hao kuzungumza na Waandishi wa Habari.
Mheshimiwa Novák ni Rais wa kwanza mwanamke kuongoza Hungary ambapo alichaguliwa mwezi Mei, 2022. Aidha, ni Rais wa kwanza kutoka Hungary kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania.