×

Waziri Mkuu wa Canada Atangaza Kutengana na Mkewe Sophie Grégoire

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau ametangaza kutengana na mkewe Sophie Grégoire (48) baada ya kudumu naye kwenye ndoa kwa muda wa miaka 18 tangu walipofunga ndoa mnamo mwaka 2005.

Wanandoa hao wenye ushawishi mkubwa kisiasa ambao mahusiano yao yalianza tangu wakiwa shuleni wamefikia uamuzi huo baada ya mazungumzo mengi yenye maana na magumu.

Hata hivyo wawili hao ambao tayari wametia saini makubaliano ya kisheria ya kutengana, kwa kauli ya pamoja wamesema “wanasalia kuwa familia yenye ukaribu na yenye upendo mkubwa na heshima kwa kila mmoja na kwa kila kitu ambacho wamejenga na wataendelea kujenga.”

Waziri Mkuu huyo na mke wake huyo ambao tayari wamesaini makubaliano ya kutengana wana watoto watatu, Xavier (15), Ella Grace (14) na Hadrien (9).

EXCLUSIVE: ABDULRAZAK AFICHUA ya DIVA, UGOMVI,SHIDA ya KUPATA MTOTO, AWATAJA SUMA LEE, CHIFU KIUMBE

Leave a Comment