
KAMPUNI ya Societe Petroliere Rwanda, imepiga hatua kubwa kwa kufungua tawi la kwanza nchini Tanzania, ikiashiria dhamira yake ya kuwa mtoa huduma mkuu wa suluhu za petroli wakati wa kuwasilisha bidhaa zinazojali mazingira.
Kuanzishwa kwa SP Tanzania, kunasisitiza azma ya kampuni hiyo kuibua mambo mapya ya masoko na kutoa huduma ya kipekee kwa wateja wake wanaokua kila mara.
Tawi hilo la Tanzania linakuwa sehemu ya matawi mengine katika nchi kadhaa za Afrika ikiwemo vituo 64 vya huduma nchini Rwanda na 18 nchini Morocco.
Shauku ya Societe Petroliere Rwanda, inachochewa zaidi na eneo la kimkakati la ambapo SP Kibaha ina uwezo mkubwa, sio tu kuhudumia soko la ndani, bali pia ina jukumu muhimu katika kuwezesha biashara za mipakani kati ya Rwanda na Tanzania.
Hii ni nafasi bora itatumika kama msingi muhimu wa vifaa kwa wasafirishaji, kukuza uchumi wa kikanda. Hatua hii inaonyesha maono ya kampuni ya kuunda matokeo chanya nje ya mipaka ya Rwanda, ikikumbatia ukuaji na ushirikiano wa kikanda.
Yves Legrux, Mkurugenzi Mtendaji wa SP Rwanda, alisema: “Leo ni hatua muhimu kwa Societe Petroliere. Baada ya kuzindua oparesheni mpya huko Morocco wiki chache zilizopita, ni kwa fahari kubwa kwamba tunazindua kituo chetu cha kwanza cha mafuta nchini Tanzania.
“Iko kwenye barabara ya kwenda Rwanda, eneo hili linawakilisha eneo linalofaa kwa kiingilio cha soko cha SP. Kutoka eneo hili, tunaangalia mbele Zaidi kwa kuwapa wateja uzoefu wao wa kwanza wa Rwanda wanapokuwa njiani. Tuna hakika kwamba kituo hiki haitakuwa mwisho, tunatazamia kwa mengi zaidi.”