×

Baba wa Ngusa Samike Azikwa Kahama

Leo Januari 25, 2022, baba wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ngusa Samike, Mzee Fredrick Shija Samike amezikwa katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Katika ibada ya maziko, Waziri wa Tamisemi, Innocent Bashungwa ametoa salamu za pole kwa Rais Samia Suluhu Hasaan.

“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amenituma kwa niaba yake na Serikali kutoa salamu za pole kwa familia na ninatoa pole kwa kaka yangu Ngusa kwa pengo kubwa la mzee wetu tulilolipata” amesema Bashungwa.

Waziri Bashungwa ametoa wito kwa ndugu jamaa na marafiki kuendelea kumuombea Mzee Samike huku akisisitiza umuhimu wa wananchi Mjini Kahama na kwingineko kujifunza na kuyaenzi maisha ya mzee Samike.

Aidha, Waziri Bashungwa amepata nafasi ya kutoa mkono wa pole kwa niaba ya Serikali vilevile Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa familia.

Katika msiba huo Waziri Bashungwa ameambatana na Waziri wa Madini Mhe Dkt Doto Biteko, Naibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis H. Khamis na Wakuu wa Mikoa ya Shinyanga na Mwanza.

Mzee Fredrick Shija Samike alifariki tarehe 20 Januari 2022 katika hospitali ya Bugando iliyopo Jijini Mwanza alipokuwa akipatiwa matibabu na mwili wake umepumzishwa nyumbani kwake Kahama.

Leave a Comment