
UONGOZI wa Simba, umebainisha kuwa, balaa la nyota wa kikosi hicho kinachofundishwa na Roberto Oliveira kwa msimu mpya ni zito.
Julai 12, 2023, msafara wa Simba uliibukia Uturuki kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu wa 2023/24, kisha Agosti 2, 2023, walirejea Dar kuendelea na maandalizi mengine kuelekea Simba Day Agosti 6, 2023 na michuano mingine.

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, alisema Clatous Chama, Luis Miquissone na Fabrice Ngoma, wapo imara kuwapa burudani.
“Wote waliopo ndani ya Simba ni wachezaji wa mpira, uwepo wao katika kikosi unaongeza tabasamu. Fikiria una Chama, Ngoma, Luis, hapo sijamtaja Kibu Denis, Jean Baleke, unadhani nini kitatokea? Hili ni balaa kwelikweli.
“Kila mchezaji anatambua namna Wanasimba wanapenda kuona wanacheza vizuri na kupata matokeo kwenye mechi zote za ushindani, ni muda wa kuendelea kuwa pamoja na kila kitu kitakuwa sawa,” alisema Ally.