×

Mbeya yafurika banda la Lake Gas Nanenane

Wakazi wa Mkoa wa Mbeya wamefurika katika banda la kampuni ya Lake Gesi lililopo katika viwanja vya nanenane mkoani humo kununua  majiko na mitungi ya  gesi inayouzwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati vijijini(REA) kwa Bei ya Punguzi katika viwanja vya Maoneesho hayo ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Akizungumza katika viwanja hivyo  Menena Masoko na Mawasiliano wa  Lake Energies Group,Matina Nkurlu alisema wao kama  kampuni wamekuja na kampeni mpya ya”Pika na Pakua na  Lake gesi” ikiwa ni hatua ya kuunga mkono Kampeni ya Rais,Mama Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wanamshusha Mama kuni kichwani na kuhakikisha matumizi ya Gesi kwa kupikia yanaenea nchi mzima.
Katika kuhakikisha hilo Lake Energies kwa kushirikiana na   Wakala wa Nishati vijijini(REA) Tunahakikisha tunawafikia wanawake nchi nzima na kwa sasa tumeanzia mkoa wa Mbeya napenda tu kuwahakikishia wakazi wa mkoa huu kuwa tuna mzigo wakutosha na kama unavyoshuhudia  alisisitiza Nkurlu.
Nae mmoja wa kinamama anayejishughulisha na Biashara ya Mama Lishe, Atupelile Mwakakasita alisema wanaishukuru serikali kupitia REA na kampuni ya Lake Energies  kwa kuwafikia wananchi wa kipato cha chini kwa kuwaletea promosheni hii ya kuuza mitungi midogo kwa gharama nafuu.
Maonesho ya Nanenane yalifunguliwa tarehe Moja mwezi huu na Makamo wa Rais, Dkt Isdori Mipango  yanayotarajiwa kufungwa tarehe 10 mwezi huu.

Leave a Comment