Binti Zaidina Issa 29 ambaye ni mama wa watoto 3 Mkazi wa kijiji cha Diloda Halmashauri ya wilaya Hanang’ Mkoani Manyara Ameiomba Serikali pamoja na wasamaria wema kumchangia fedha kwaajili ya kwenda kufanyiwa upasuaji wa uvimbe tumbo aliokuwanao pamoja na TB ya Mapafu pamoja na kufanyiwa uchunguzi wa tatizo la figo.
Akizungumza na Global Online Tv Zaidina amesema kutokana na maradhi aliyokuwanayo kwa muda mrefu ameshidwa kufanya kazi ili kujikimu kimaisha huku akieleza kuwa alifanikiowa kuolewa lakini Aliachwa na mumeo kutokana na Maradhi hayo.
Kwa Mawasiliano zaidi au msaada unaweza kutuma Mchango wako Kupitia Namba 0756 889 168 Jina Safina Issa Mwangu ambaye ni Mama yake mzazi anayemuuguza.