×

Afrika Kusini: Jacob Zuma Aondolewa Hukumu ya Kifungo cha Miaka 15

Hukumu ya kifungo cha miezi 15 jela ya rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma imeondolewa.

Hii inamaanisha kuwa hatatumikia kifungo gerezani baada ya kuachiliwa chini ya uangalizi wa magereza.

Mwandishi wa Johannesburg Nomsa Maseko Mahakama Kuu ya Rufaa iliamua kwamba kuachiliwa kwake kwa msamaha wa matibabu ilikuwa kinyume cha sheria na ni batili.

Kamishna wa Magereza wa Afrika Kusini Makgothi Thobakgale amesema kuwa Jacob Zuma aliripoti katika kituo cha Estcourt Correctional katika jimbo lake la Kwa Zulu natal asubuhi ya leo na “aliingizwa” katika mfumo huo.

Aliachiwa saa moja baadaye chini ya mchakato maalum wa msamaha. Hali ya msamaha iliidhinishwa na Rais Cyril Ramaphosa kwa wafungwa zaidi ya elfu tisa walio katika hatari ndogo.

Waziri wa sheria Ronald Lamola alisema uamuzi huo ulichukuliwa ili kushughulikia msongamano wa wafungwa katika magereza na kwamba mchakato huu wa msamaha ulianza mwezi Aprili.

Zuma alihukumiwa kifungo cha miezi 15 mwaka 2021 kwa kudharau mahakama, kwa kukataa kutoa ushahidi katika uchunguzi wa mahakama kuhusu ufisadi wa serikali wakati wa muhula wake wa uongozi.

Kufungwa kwake kulizua ghasia zilizosababisha vifo vya watu 350 na mamia ya biashara kuporwa na kuchomwa moto.

WAFUGAJI WAASWA KUTUNZA MAENEO ya MALISHO ILI KUEPUSHA MIGOGORO KWENYE HIFADHI WAKATI wa KIANGAZI

Leave a Comment