×

Ikiadhimisha Miaka Mitano, Thamani ya Uwekezaji Mfuko wa PSSSF Yafikia sh trilioni 7.8

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa nne kulia), akikabidhi zawadi kwa Makamu Mwenyekiti  wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF, Dk. Aggrey Mlimuka wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa huduma za kidigitali za PSSSF Pamoja jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
  • Waziri Mkuu aagiza mifuko yote ya hifadhi ya jamii kulipa mafao kwa wakati
  • Huduma zinazopatikana kupitia  PSSSF Pamoja ni utaratibu wa wanachama wapya kujiunga kwenye mfuko, mfumo wa kidigitali wa kuanzisha madai ya mafao na uhakiki wa wastaafu kupitia simu janja popote walipo bila kufika kwenye ofisi za mfuko.

*PSSSF yaadhimisha miaka mitano ikizindua huduma za wanachama kidigitali

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea zawadi kutoka kwa Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (wa tatu kushoto) wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja uzinduzi wa huduma za kidigitali za PSSSF Pamoja jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Huduma zinazopatikana kupitia  ‘PSSSF Pamoja’ ni utaratibu wa wanachama wapya kujiunga kwenye mfuko, mfumo wa kidigitali wa kuanzisha madai ya mafao na uhakiki wa wastaafu kupitia simu janja popote walipo bila kufika kwenye ofisi za mfuko. Wengine kutoka kulia ni, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo, CPA. Hosea Kashimba na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF, Mhandisi Musa Iyombe.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa huduma za kidigitali ya PSSSF Pamoja,  wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa huduma za kidigitali za mfuko huo  jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wahudhuriaji wakishiriki maadhimisho ya miaka mitano ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa huduma za kidigitali za PSSSF Pamoja jijini Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, viongozi wa Mfuko wa PSSF, viongozi wa kiserikali wa mkoa wa Dodoma pamoja na wahuduriaji wengine mashuhuri wakipozi kwa picha ya kumbukumnbu mara baada ya maadhimisho ya miaka mitano ya PSSSF

Leave a Comment