×

Familia Iliyopoteza Watu Watano Kwa Kuungua Na Moto Huzuni Tupu!

Kutoka kulia ni baba wa familia, Edward Jeremiah Katema aliyeondokewa na wapendwa wake watono katika ajali ya moto uliotokea nyumbani kwake. Anayemfuatia kulia kwake ni mwanaye, mdogo wake wa kike na kushoto anayoonekana ni mwandishi wa habari wa Global Tv Online.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa familia ya Katemi kuombolezavifo vya wanafamilia watano.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwenye familia iliyopoteza wapendwa wao watano. 
Nyumba iliyoungua.

Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wamefika nyumbani kwenye familia ya watu wa tano ya , Edward Jeremiah Katema waliopoteza maisha katika ajali ya moto kwa ajili ya kutoa pole na kuendelea shughuli nzima za maombolezo.

Katemi akizungumzia chanzo cha vifo hiyvyo alisema kuwa ni kutokana na hitilafu ya umeme uliopelekea  kuunguza nyumba yao na kusababisha vifo vya wanafamilia hiyo.

Amesema kuwa wakati akitokea katika shugghuli zake majira ya saa nne usiku ndipo alikutana na janga hilo la moto ambapo walifanya juhudi za kuwaokoa lakini kwa bahati mbaya ilishindikana kutokana na kuwa tayari walikuwa wameumia sana lakini walifanya juhudi za kuokoa uhai wao kwa kuwapeleka hospitalini lakini walipoteza maisha.

Akizungumzia taratibu za mazishi ,Jeremiah  amesema taratibu za kuhifadhi miili hiyo inaendelea na lakini taratibu za awali wanatarajia kusafirisha miili hiyo hadi Buchosa-Sengerema Mwanza katika kijiji cha Sukuma kata ya Bukokwa.

Leave a Comment