×

Mama Lishe Aondoka Na Milioni Moja Ya Tigo Chawote, Wengine Nao Wajizolea Milioni Milioni Zao

Mary Audax Rutta Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa

Dar es Salaam, 17 Agosti 2023: Ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya chawote ya kampuni ya tigo mpaka sasa imefikia zaidi ya washindi elfu kumi na saba.

Hayo  ameyasema  Mary Audax Rutta Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa leo Agosti 18,2023 wakati akikabidhi hundi ya shilingi milioni moja kwa washindi hao Jijini Dar es Salaam iliyoshuhudiwa na waandishi wa habari.

Joyce Massaba Mkazi wa Dar es Salaam.

Kwa upande wake Joyce Massaba Mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni mshindi wa milioni moja amesema  fedha hizo zitamsaidia kwenye malengo ya kibiashara  anayotarajia kuyafanya.

Nae Amina Rajabu Mkazi wa Dar es salaam mshindi wa milioni moja ameongezea kwa kusema   fedha hiyo itamsaidia kwenye biashara yake ya mama lishe  kuongezea mtaji wake na kukuza biashara hiyo.

Mama Lishe Amina Rajabu akiwa kwenye pozi la furaha kwenye hafla ya kukabidhiwa pesa yake.

Sanjari na hayo mshindi mwingine wa milioni moja, Godfrey Tarimo mkazi wa Dar es Salaam amesema  hela hiyo itamsaidia katika mambo yake mengine binafsi.

Promosheni hiyo ya chawote itadumu kwa siku tisini hii ikiwa  ni wiki ya nane mshindi wa mwisho wa mwezi anashinda milioni tano mbali na zawadi za fedha taslim wanazotoa nyingine ni bonus, dakika na sms.

Leave a Comment