×

Majembe Ya Simba Wameanza kwa Majanga Msimu wa 2023/24

Aubin Kramo ingizo jipya kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

MASTAA watatu wa Simba, wameanza kwa majanga msimu wa 2023/24 kutokana na kupata maumivu wakiwa kwenye majukumu yao.

Miongoni mwao ni pamoja na Aubin Kramo, huyu ni ingizo jipya kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast aliyepata maumivu akiwa mazoezini.

Nyota huyo hajacheza mchezo wowote ndani ya kikosi cha Simba kuanzia Ngao ya Jamii pamoja na Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, uliochezwa Uwanja wa Manungu.

Beki wa kati, Henock Inonga, alipata maumivu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate ikiwa ni hatua ya nusu fainali alipogongana na mshambuliaji, Meddie Kagere dakika ya 90.

Mkandaji, Kibu Denis kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar, alipata maumivu dakika ya 75, akakwama kukamilisha dakika 90, nafasi yake ikachukuliwa na Moses Phiri.

Taarifa kutoka kwa Daktari wa Simba, Edwin Anakret Kagabo, zimeeleza kuwa, wachezaji hao wanaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.

“Wachezaji wanaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu, hivyo kinachoendelea kwa sasa ni uangalizi ili wawe imara kwa ajili ya kuendelea na majukumu yao,” alisema daktari huyo.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

#HIGHLIGHTS: PENALTY za ROBO FAINALI SHIGONGO CUP, KALEBEZO ( 4 ) vs LUGATA ( 3 )…

Leave a Comment