
PICHA mpya kutoka eneo la Tver nchini Urusi, ambako wataalamu wa masuala ya dharura na polisi wanachunguza mabaki ya ndege ya kibinafsi iliyohusishwa na kufariki kwa Kiongozi wa kundi la Wagner ambaye ni mpinzani mkubwa wa Rais Vladimir Putin wa Urusi, Yevgeny Prigozhin.
Ikulu ya Kremlin bado haijathibitisha iwapo mkuu wa Wagner alifariki katika ajali ya ndege jana, lakini maafisa wa anga walisema alikuwa mmoja wa abiria sita waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Maafisa wa anga wa Urusi walithibitisha kuwa ndege hiyo, Embraer Legacy, ilikuwa ikisafiri kati ya Moscow na St Petersburg ilipoanguka katika eneo la Tver, kaskazini mwa Moscow Jumatano jioni.
Ndege hiyo ya kibinafsi ilikuwa imebeba abiria saba na wahudumu watatu.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, watu wote 10 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliuawa. Miili yote inasemekana kupatikana.
Ndege hiyo ya Embraer Legacy – iliyosajiliwa na moja ya kampuni za Prigozhin – iliwaka moto ilipogonga ardhi baada ya kuripotiwa kuwa angani kwa chini ya nusu saa.



