
Utaratibu huo ambao si wa kawaida umefanyika kutokana na baadhi ya Kata zilizopangiwa kukamilisha zoezi hilo kwa siku moja, kuchelewa kupata Karatasi za Kupigia Kura na baadhi ya Vituo Kuchelewa kufunguliwa
Maeneo yaliyopata changamoto ni Harare na Bulawayo ambako ni ngome za Upinzani chini ya mgombea wake Nelson Chamisa ambaye amemtaja Rais Emmerson Mnangagwa kuhusika na hujuma hiyo na kueleza kuwa anatumia njia za kizamani kuvuruga Uchaguzi
Zimbabwe inafanya Uchaguzi wa 9 tangu ilipopata Uhuru mwaka 1980, Wagombea 11 wanawania Kiti cha Urais akiwemo Rais Mnangangwa aliyeingia madarakani kwa kumpindua Hayati Robert Mugabe na Mwanamke mmoja.