×

Waziri Mkuu Majaliwa: Serikali Itaendelea Kumuenzi Marehemu Bernard Membe

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Agosti 26, 2023 ameshiriki kwenye ibada ya kumbukumbu ya Marehemu Bernard Membe iliyofanyika katika kijiji cha Rondo, Mkoani Lindi.

Akizungumza na waombolezaji Kassim Majaliwa amesema kuwa weledi, nidhamu, uchapakazi na umahiri wa Marehemu Membe uliitambulisha Tanzania katika medani za kimataifa na kuisaidia nchi yetu kutengeneza marafiki na mataifa mengine.

Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuyaenzi mambo yote mazuri yaliyofanywa na marehemu, Bernad Membe wakati wa utumishi wake Serikalini.

Marehemu Membe ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje alifariki dunia Mei 12 mwaka huu katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Leave a Comment