×

Mchungaji Akamatwa Kwa Kutengeneza Tukio La Uongo La Kishirikina Kuwalaghai Waumini – Video

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu wawili akiwemo mchungaji wa Kanisa la Pentecoste Gospel Mission lililopo lililopo Kibaha mkoa wa Pwani kwa tuhuma za kutengeneza tukio la uongo la kishirikina ili kuwalaghai waumini wa kanisa hilo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amesema Agosti 24, 2023 majira ya saa 09:00 asubuhi, huko katika kituo cha polisi kibaha Mkoa wa Pwani, Emanurl Paul almaarufu Karata (35), Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Gospel Mission lililopo kibaha alitoa taarifa za mtu mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Basenga Matheo (59), Mkazi wa Miswe Wilaya ya Kibaha akiwa amesafiri kwa ungo wa kishirikina na
kudondoka kanisani hapo na kuleta taharuki kubwa kwa waumini.

Katika uchunguzi, Jeshi la Polisi lilibaini kuwa tukio hilo ni tukio la kutengeneza kwa lengo la kuwalaghai au kuwahadaa waumini na wananchi kwa jumla kwa
lengo la kupata waumini zaidi na kujipatia kipato.

Busenga alijinisabu kuwa yeye na
wenzake walifika kanisani hapo kishirikina kwa lengo la kupima Imani ya waumini hao kwa mwenyezi mungu.

Aidha mtuhumiwa aliahidiwa kulipwa Tsh. 50,000/=
baada ya kutimiza lengo lao la kilaghai.

Leave a Comment