
Rais Samia Suluhu Hassan amemvua hadhi ya ubalozi Dkt. Willibrod Slaa kuanzia hii leo, Septemba Mosi.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imethibitisha utenguzi huo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Dkt. Slaa aliteuliwa kuwa balozi Novemba 23, 2017, na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli na kupangiwa kituo cha kazi nchini Sweden.

