
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kupitia kwa Kamanda wa Mkoa, RPC Pius Lutumo limetolea ufafanuzi sakata la binti mdogo, Warda Mohammed (15), mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyumbu, Kibaha kupotea tangu April 19, 2023.
Kamanda Lutumo amesema walipokea taarifa za kupotea kwa binti huyo kutoka kwa mtoto wa mwalimu aliyekuwa akiishi naye ambapo jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini mahali alipo mwanafunzi huyo.
Kamanda Lutumo amesema matukio ya wasichana wa umri kama wa Warda kupotea, yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara na kutoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zinazoweza kupatikana kwa binti huyo, aziwasilishe kwenye mamlaka yoyote anayoiamini.