
LEO Jumapili, fainali ya michuano ya Ndondo Cup 2023, inatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Kinesi uliopo Shekilango, Ubungo, Dar, kati ya Madenge FC kutoka Magomeni-Makuti Wilaya ya Kinondoni, dhidi ya Kibangu Rangers inayotokea Kibangu Wilaya ya Ubungo.
Madenge imeingia Fainali ya Ndondo Cup kwa mara ya pili mfululizo baada ya msimu uliopita kufanikiwa kuwa mabingwa, huku Kibangu Rangers inaweka historia ya kucheza fainali ya Ndondo Cup kwa mara ya kwanza tangu ilipoanza kushiriki mashindano hayo.
Mratibu wa Ndondo Cup, Yahya Mohamed ‘Mkazuzu’ amesema, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Hamis Mwinjuma, anatarajiwa kuwa mgeri rasmi kwenye fainali hiyo.
Kuelekea fainali hiyo, Nahodha Msaidizi Madenge, Mashaka Pogba, alisema: “Wapinzani tunaokutana nao ni ndugu zetu, wanasema rekodi haivunjwi, lakini sisi tunavunja rekodi yetu wenyewe.”
“Hili kombe halijawahi kuchukuliwa mara mbili na timu moja, lakini kesho (leo) sisi tutalichukua kivyovyote,” aliongeza Nahodha Mkuu wa Madenge, Diye Makonga.
Kwa upande wa Kibangu Rangers, nahodha wa timu hiyo, Mushda Hamis, amesema: “Kwa niaba ya wachezaji wenzangu tumejiandaa, mimi nimeanza kushiriki mashindano haya tangu mwaka wa kwanza nikiwa na Makumba FC, lakini sijawahi kuingia fainali, lakini kesho (leo) nitajitoa kuhakikisha tunabeba ubingwa kwani itakuwa faraja kwangu mara ya kwanza naingia fainali na kuchukua kombe.”
SIMBA vs AHLY: AHMED ALLY BAADA ya KUPANGIWA AHLY AFL CHEKI TAMBO ZAKE…