Waziri Mkuu Atoa Maelekezo Kwa Doto Biteko Sakata la Mafuta – (Picha + Video)
Global Publishers September 7, 2023 0 Comments
SHARE THIS:
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko kwenye sekta ya mafuta.
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 7, 2023 alipokuwa anajibu maswali ya papo kwa hapo kutoka kwa wabunge katika kipindi cha asubuhi.
Katika swali la msingi, Mbunge wa Lushoto (CCM) Rashid Shangazi alitaka kujua Serikali inaweka mkakati gani kuhakikisha upatikanaji wa mafuta unakuwa ni mzuri nchini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza swali kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum, Hawa Mwaifunga, wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma, Septemba 7, 2023.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Urambo Margaret Sitta, bungeni jijini Dodoma, Septemba 7, 2023.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Septemba 7, 2023. Katikati ni Mbunge wa Mikumi, Dennis Londo.