×

Tecno Camon 16 Waja na Zawadi Kwa Wateja Ikinogeshwa na App ya Vskit

Meneja Mauzo wa Tecno hapa nchini, Mariam Mohammed akionesha saa itakayotolewa kama promosheni pamoja na boksi lake.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tecno katika kuelekea msimu wa Sikukuu ya Krismasi imekuja na ofa kabambe kwa wateja wake watakaonunua toleo lao jipya la Camon 16 huku ofa hiyo ikinogeshwa na App ya Vskit iliyomo kwenye simu hiyo.

Katika uzinduzi wa promosheni hiyo Meneja Mauzo wa Tecno Tanzania, Mariam Mohammed amesema kwa mteja yeyote atakayenunua simu hiyo kwenye duka lolote hapa nchini atapata zawadi ya saa ya kidijitali (Smart watch).

Meneja wa App ya Vskit hapa nchini Paulina Luhai (kushoto) na afisa mwenzake wakionesha fulana yenye nembo ya App hiyo. 

Baada ya meneja huyo kusema hayo naye, Meneja App ya Vskit hapa nchini Paulina Luhai amesema App hiyo ambayo pia inapatikana kwenye simu janja zingine za Tecno matoleo ya kisasa ndiyo jibu sahihi ya kuedit picha kwenye simu yako na kuzipa ubora unaohitaji.

Paulina amesema wajanja wengi wa masuala ya kuedit picha za mnato na video kwasasa wamekuwa wakitumia program zilizomo kwenye App hiyo kuedit picha zao.

Meneja Uhusiano wa Tecno, Eric Mkomoye (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa Vskit na ofisa mwenzake wa Tecno (Wapili kutoka kulia).

“Kwa wanaopenda kuedit picha na video kupitia simu zao App ya Vskit ambayo ni rahisi kutumia ndiyo kila kitu hivyo wajaribu kuitumia kuanzia sasa wajionee wenyewe”. Alimaliza kusema Paulina.

Leave a Comment