×

ATCL Yasitisha Safari za Tanzania Kwenda Guangzhou Nchini China hadi Oktoba

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imesitisha safari za Tanzania kwenda Guangzhou nchini China hadi Oktoba 16, 20213 kutokana na suala la kiufundi

Akibainisha hilo, Anna Paul kutoka kituo cha mawasiliano na huduma kwa wateja wa Kampuni hiyo amesema wateja waliokwisha kata tiketi zao watasafiri kupitia Shirika la Ndege la Qatar.

Safari za ndege za abiria kutoka Tanzania kwenda Guangzhou, China zilirejea rasmi Julai 17, 2022 baada ya kusitishwa kwa muda kutokana na janga la UVIKO- 19 ambalo lilibuka mwishoni mwa mwak 2019 na kuleta athari kubwa ulimwenguni ikiwemo vifo.

China na Tanzania ni washirika wazuri wa kibiashara. Pia nchi hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania ikiwemo kuboresha miundombinu.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHTUKIA UPIGAJI FEDHA KIGOMA, AUNDA TIMU ya UCHUNGUZI…

Leave a Comment