
KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel gamondi, ameweka wazi kuwa, watu wengi waliona kuwa timu yake ingeweza kupata shida bila ya uwepo wa Fiston Kalala Mayele jambo ambalo kwake alikuwa hakubaliani nalo.
Mayele kabla ya kuondoka Yanga na kutua Pyramids ya Misri, alikuwa ndiye mshambuliaji tegemeo wa klabu hiyo kwa misimu miwili, huku Gamondi akiwa hajafanikiwa kufanya naye kazi.
Akizungumza na Spoti Xtra, Gamondi alisema: “Watu wengi waliamini kuwa Yanga tungepitia wakati mgumu sana kutokana na kuondoka kwa Fiston Mayele, lakini niwaambie kuwa tayari mipano ya timu ilikuwa ipo katika njia nyingi tofauti.

“Mayele alikuwa ni mshambuliaji mzuri kweli, lakini timu lazima iwe na muundo sahihi wa kucheza bila kumtegemea mchezaji yeyote, na hiyo inakuwa ni njia nzuri kwa kuwa wachezaji huja na kuondoka, lakini timu inabaki kuwa milele.
“Tunao washambulaji wazuri ndani ya Yanga, yupo Clement Mzize, ni mshambuliaji chipukizi mzuri na anafanya vyema, Musonda na Konkoni pia, hawa kwa pamoja wanafanya kazi nzuri na naamini watatupa kile nkilicho bora,” alisema kocha huyo.
STORI NA MARCO MZUMBE