
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Maganga M. Japhet, na baadaye kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera lakini hakuitumikia nafasi hiyo, ametakiwa kurejea kwenye majukumu ya Ualimu mara moja kuanzia Oktoba 1, 2023
Anarejea kwenye Cheo cha Mwalimu Mwandamizi Daraja A katika Manispaa ya Temeke baada ya maombi yake ya kuongeza muda wa kuazimwa kukataliwa. Awali aliomba kibali cha kuazimwa kuitumikia CWT (Agosti 21, 2017 hadi Septemba 30, 2020), akaomba tena Juni 1, 2020 na anamaliza muda wake Septemba 30, 2023, Mwalimu Maganga aliomba kibali kingine kwa mara ya tatu ndipo kimekataliwa.