×

Mwandishi na Mhariri Mtendaji, Saleh Ally Aweka Rekodi Mpya FIFA

Mwandishi mkongwe wa michezo nchini, Saleh Ally, maarufu kama Salehjembe.

Mwandishi mkongwe wa michezo nchini na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally, maarufu kama Salehjembe, ameandika rekodi nchini

ya kuwa mwandishi wa kwanza kupiga kura mara nne mfululizo katika tuzo za The Best FIFA Football Award.

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), limemchagua tena Salehjembe, kupiga kura katika tuzo za mwaka 2023

ambazo hutoa mwanasoka bora wa dunia.

Kawaida katika kila nchi hutolewa nafasi kwa Kocha wa timu ya taifa, nahodha wa timu ya taifa na waandishi

wa Habari kupiga kura hizo muhimu.

Salehjembe ameandika rekodi hiyo ikiwa ni mara yake ya nnemfululizo akiteuliwa kupiga kura. Hali  inayoonyesha uaminifu mkubwa kutoka Fifa yenye makao yake makuu nchini Uswiss.

Kura atakazopiga ni vipengele sita vya The Best FIFA Women’s Player, The Best FIFA Women’s Coach, The

Best FIFA Women’s Goalkeeper, The Best FIFA Men’s Player, The Best FIFA Men’s Coach na The Best FIFA Men’s Goalkeeper.

Leave a Comment