×

Watanzania Wawili Hawajulikani Walipo Mapigano Ya Nchini Israel, Balozi Afunguka

 

Wakati mapigano yakiendelea nchini Israel kati ya Taifa hilo na kundi la wanamgambo la Hamas la nchini Palestina, imetoka taarifa mpya kutoka kwa Ubalozi wa Tanzania nchini humo juu ya Watanzania wawili ambao walikuwa ni wanafunzi wa mafunzo ya vitendo ‘internship’ kusini mwa Israel.

Balozi wa Tanzania nchini Israel, Alex Kallua amesema “Tunaendelea kuwafuatilia watanzania wawili ambao ni wanafunzi waliokuwa wanafanya mafunzo kwa vitendo kusini mwa nchi hiyo, tunafanya jitihada za kuwapata kwanza ili kufahamu walipo na hali zao,”

hali ya Watanzania wengine 350 waishio nchini humo ikiwepo wanafunzi 260 wako salama katika maeneo mbalimbali nchini humo na wamekuwa na mawasiliano na ubalozi.

Leave a Comment