
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Leo Oktoba 09, 2023 akiwa kwenye ziara yake nchini India amezuru kaburi la Hayati Mahatma Gandhi lililopo kwenye Makumbusho ya Mahatma Gandhi Rajghat New Delhi nchini India.
Mahatma Gandhi ambaye ni baba wa Taifa hilo alikuwa mwanasheria, mwanafalsafa, mwanaharakati wa haki za binadamu na kiongozi wa siasa nchini India ,Anajulikana hasa kama kiongozi wa harakati za uhuru wa India aliyepinga na kushinda Ukoloni kwa njia ya amani bila ya matumizi wa mabavu au silaha, Mahatma Gandhi ambaye alifariki January 30, 1948 akiwa na miaka 79.
Mapema leo Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake nchini humo alimgusia Mahatma Gandhi kuwa wakati wa safari yake ya kwenda nchini Afrika kusini alilala hotel kubwa Zanzibar iiitwayo Tembo House Hotel.
